The One New Heart Tanzania
A mother smiles with her child, who waves a toy from a hospital bed

Tunawasaidia watoto wenye matatizo ya moyo kupata matibabu wanayohitaji

The One New Heart Tanzania inahakikisha watoto wa Tanzania wenye matatizo ya moyo wanapata vipimo, matibabu na ufuatiliaji, huku ikiimarisha hospitali na wataalamu wanaotoa huduma hizo.

A phone shows an echocardiogram image beside a portable ECG machine

Kugundua matatizo ya moyo mapema, karibu na nyumbani

Tunapima watoto kwa echo na ECG kwenye hospitali za mikoa, ili familia isilazimike kusafiri mbali kujua tatizo la mtoto.

A child in intensive care with monitoring leads after heart surgery

Operesheni kwa watoto ambao familia zao haziwezi kumudu gharama

Madaktari wa Tanzania na madaktari wageni wanafanya operesheni pamoja kwenye hospitali tunazoshirikiana nazo.

A visiting clinician demonstrates an echocardiogram while local clinicians observe

Ujuzi unaobaki Tanzania

Kila mission pia ni darasa. Madaktari, wauguzi na mafundi wa Tanzania wanajifunza kwa vitendo pamoja na wataalamu wageni, ili ujuzi ubaki hapa nyumbani.

Clinicians and a caregiver celebrate with a child after treatment

Huduma inayoendelea baada ya operesheni

Kliniki ya ufuatiliaji na dawa kwa muda wote ambao mtoto anazihitaji.

Tatizo

Tatizo la moyo kwa mtoto linaweza kupita bila kuonekana. Kuligundua mapema kunaokoa maisha.

Takriban 1 kati ya 100

ya watoto wanaozaliwa wana tatizo la moyo tangu kuzaliwa.

Chanzo: Makadirio ya kimataifa ya magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo
2.1%

ya wanafunzi waliopimwa kwenye utafiti mmoja hapa Tanzania walikutwa na rheumatic heart disease bila kuonyesha dalili zozote.

Chanzo: Utafiti wa echocardiography mashuleni Tanzania
Upatikanaji mdogo

wa vipimo vya moyo unafanya iwe vigumu kugundua tatizo mapema, hasa nje ya miji mikubwa.

Chanzo: Ripoti ya Matokeo ya TONHT 2025 / machapisho ya huduma za moyo Tanzania

Tunachofanya

Kugundua

Uchunguzi na rufaa

Tunawapima watoto ili kuwatambua wenye tatizo la moyo, kisha tunawapa rufaa.

Kutibu

Kupata matibabu

Tunawasaidia watoto kupata matibabu sahihi ya moyo, ikiwemo operesheni na matibabu ya kibingwa.

Kuimarisha

Mafunzo na mifumo

Tunasaidia mafunzo, ushirikiano na mifumo inayoziwezesha hospitali zetu kutoa huduma bora za moyo.

Kukinga

Uelewa na kinga

Tunaelimisha jamii kuhusu magonjwa ya moyo na jinsi ya kujikinga, hasa rheumatic heart disease.

Angalia tunachofanya

Matokeo

Tangu 2019

Angalia matokeo yote

200+watoto wamepata matibabu ya moyo
1,500+watu wamepimwa kwenye kambi zetu
150+watu wamepewa rufaa kwa matibabu ya kibingwa mwaka 2025
Catherine sits on her mother’s lap beside a One New Heart awareness banner
Hadithi maalum

Walisema ni uchawi. Mama yake akampeleka kwa daktari

Catherine alikuwa na miezi mitatu mama yake alipoona anapumua haraka kupita kiasi. Majirani Musoma walisema ni uchawi. Mama yake aliendelea kuwauliza madaktari hadi akapata jibu, na tarehe 28 Mei 2026 moyo wa Catherine ulifanyiwa upasuaji Dodoma.

Soma hadithi ya Catherine

Programu maalum

Colors to Save Hearts

Tunawakinga watoto dhidi ya rheumatic heart disease kupitia shule, walimu na wahudumu wa afya.

Kuhusu programu hii

Reducing rheumatic heart disease among school children in Tanzania, Colors to Save Hearts
Video

Scarlett anaonyesha mchoro wake

Video zote

Travellers with One Heart Travel
Travel for Hearts

Safiri ukisaidia watoto

One Heart Travel ni kampuni yetu ya utalii. Asilimia 50 ya faida yake inaenda kwenye matibabu ya moyo ya watoto. Safari za wanyamapori, likizo Zanzibar, ziara za kiutamaduni na utalii wa matibabu, zote zikipangwa kwa uwajibikaji.

Panga safari na One Heart Travel

Uanachama

World Heart Federation Global Heart Hub
Jarida

Jiandikishe kupata habari zetu

Habari za mission zetu, hadithi za watoto na ripoti zetu, mara chache kwa mwaka. Hatumpi mtu yeyote barua pepe yako, na unaweza kujiondoa wakati wowote kwa bofya moja.

Lugha